Upambanuzi wa Miundo ya Toponemia katika Jamii: Mfano kutoka Jimbo Dogo la Maara nchini Kenya
View/ Open
Date
2022Author
Mutegi, David Micheni
Mugambi, Allan
Kinoti, Timothy M.
Metadata
Show full item recordAbstract
Makala hii imewasilisha uchunguzi uliofanywa kuhusu michakato na mbinu
zilizotumika katika uundaji wa toponemia katika jamii. Lengo mahsusi la utafiti huu
lilikuwa kupambanua miundo ya toponemia katika eneo la Mwimbi na Muthambi
jimboni dogo la Maara. Maeneo haya yaliteuliwa kwa vile yalihusiana kilugha na
kiutamaduni hasa katika suala la onomastiki. Nadharia ya Ujinaishaji ndiyo ilitumiwa
kuongoza utafiti huu. Data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kupitia kwa ya mahojiano ya
ana kwa ana pamoja na hojaji. Mahojiano yalimwezesha mtafiti kupata data ya kutosha
na halisi moja kwa moja kutoka kwa wahojiwa. Hojaji ilimwezesha mtafiti kukusanya
data kwa urahisi katika maeneo mengi na kutoka kwa sampuli kubwa. Walengwa katika
utafiti huu walikuwa wakaazi wa Mwimbi na Muthambi. Usampulishaji ulifanywa
kimaksudi kwa kuhusisha machifu 5 wa kata 5 za Mwimbi na Muthambi na manaibu wa
chifu 25 kutoka kata ndogo 25 za eneo hili. Watawala hao walichaguliwa kwa sababu
wao ni wenyeji wa eneo hili walio na habari kuhusu maeneo yao ya utawala, na hivyo
wangetoa habari kamilifu kuhusu maswali ya utafiti. Sampuli nyingine ya Wazee 20
wenye umri wa miaka sabini na zaidi walichaguliwa kimakusudi kwa kutumia mbinu ya
kimtandao ili kutoa habari kuhusu michakato ya uundaji wa toponemia za shule za
msingi katika eneo la Mwimbi na Muthambi. Sampuli ya wazee iliweza kupatikana kwa
urahisi kwa sababu ndio wanaopata pesa za wazee na walijulikana katika vijiji vyao.
Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo
kulingana na madhumuni na swali la utafiti. Matokeo ya utafiti huu ni marejeleo muhimu
kwa watafiti wengine watakaoshughulikia vipengele vya onomastiki katika lahaja ya
Kimwimbi na Muthambi. Aidha, utafiti huu ulibainisha michakato mbalimbali ya
uundaji wa toponemia katika jamii.